1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroIran

Iran: Tutashambulia kambi za Marekani ikiwa tutashambuliwa

7 Februari 2026

Iran imesema itashambulia kambi za kijeshi za Marekani zilizopo Mashariki ya Kati ikiwa itashambuliwa na vikosi vya Marekani ambavyo vimepiga kambi katika eneo hilo la Mashariki ya Kati.

Waziri wa mambo ya nje wa Iran Abbas Araghchi
Waziri wa mambo ya nje wa Iran Abbas AraghchiPicha: Khalil Hamra/AP Photo/picture alliance

Haya yamesemwa leo na waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo Abbas Araghchi ambaye ameongeza kuwa hatua hiyo haipaswi kuchukuliwa kuwa shambulizi dhidi ya nchi kunakopatikana kambi hizo.

Araghchi  amesema hayo wakati wa mahojiano na kituo cha televisheni cha Al Jazeera siku moja baada ya Tehran na Washington kuahidi kuendelea na mazungumzo ya nyuklia yasio ya moja kwa moja kufuatia kile ambacho pande zote mbili zimetaja kuwa mazungumzo chanya ya Oman hapo jana.

Mwanadiplomasia huyo mkuu wa Iran amesema shambulio jipya la Marekani litajibiwa kwa matokeo sawa na hayo, huku akiongeza kuwa haitakuwa rahisi kushambulia ardhi ya Marekani lakini watalenga kambi za nchi hiyo katika mataifa ya kanda hiyo na wala sio nchi zenyewe.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW