MigogoroMashariki ya Kati
Iran yasema itaunga mkono mazungumzo ya amani Lebanon
15 Novemba 2024Matangazo
Hayo yamesemwa hivi leo na Ali Larijani, mshauri mkuu wa Kiongozi Mkuu wa Iran Ali Khamenei, amesisitiza kuwa Tehran haina nia ya kuhujumu mazungumzo hayo.
"Hatuna nia ya kuvuruga chochote. Tunalenga kuupatia suluhisho mzozo uliopo. Kwa hali yoyote ile, tunasimama na watu wa Lebanon na kuwaunga mkono. Wanaoleta usumbufu ni Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na washirika wake. Tujaribu kuwatambua marafiki na maadui zetu.”
Larijani alikutana kwa mazungumzo mjini Beirut na Waziri Mkuu wa Lebanon Najib Mikati pamoja na Spika wa Bunge Nabih Berri, huku akisisitiza kuwa Iran itaendelea kuliunga mkono kundi la Hezbollah.