1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIran

Iran yasema Marekani yashambuliwa kufuatia sera zake mbaya

30 Oktoba 2023

Iran imesema mashambulizi dhidi ya vikosi vya Marekani nchini Iran na kwengineko katika kanda hiyo yamesababishwa na sera mbaya za nchi hiyo.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Iran Nasser Kanani, amesema wanataraji Marekani itarekebisha sera zake mbaya katika ukanda huo  ambazo zinaiponza nchi hiyo.
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Iran Nasser Kanani, amesema wanataraji Marekani itarekebisha sera zake mbaya katika ukanda huo  ambazo zinaiponza nchi hiyo.Picha: jamaran

Iran imesema miongoni mwa sera hizo mbaya ni pamoja na kuiunga mkono Israel katika vita vyake dhidi ya kundi la Hamas.

Vikosi vya Marekani vimeshambuliwa mara kadhaa nchini Iraq na Syria tangu wanamgambo wa Hamas walipoingia Israel Oktoba 7 na kufanya mashambulizi yaliyouwa Waisraeli 1,400 na 239 kutekwa nyara.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Iran Nasser Kanani, amesema wanataraji Marekani itarekebisha sera zake mbaya katika ukanda huo  ambazo zinaiponza nchi hiyo.

Iran inayoliunga mkono kundi la Hamas imekanusha kuhusika na shambulio la Oktoba 7.

Marekani ina wanajeshi kiasi ya 2,500 nchini Iraq na takriban 900 nchini Syria kama sehemu ya juhudi zake ya kuzuia kuimarika tena kwa kundi linalojiita dola la Kiislamu.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW