1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIran

Iran yasema mashambulizi mapya dhidi yake 'yatashindwa tena'

23 Oktoba 2025

Iran imetahadharisha kuhusu mashambulizi mapya ya kijeshi dhidi yake na kusema 'yatashindwa tena'.

Kiongozi mkuu wa kidini wa Iran Ayatollah Ali Khamenei
Kiongozi mkuu wa kidini wa Iran Ayatollah Ali KhameneiPicha: Office of the Iranian Supreme Leader/AP/picture alliance

Tahadhari hiyo imetolewa baada ya Shirika la Umoja wa Mataifa linalosimamia nishati ya Atomiki kuelezea hofu ya uwezekano wa ‘matumizi mapya ya nguvu' ikiwa juhudi za kidiplomasia na Tehran zitagonga mwamba.

Mnamo katikati ya Juni, Israel ilifanya mashambulizi ambayo hayajawahi kushuhudiwa dhidi ya Iran, na kusababisha vita ambapo Iran ilijibu kwa makombora na droni. 

Wakati wa mzozo huo wa Israel na Iran, vita hivyo vilivyodumu kwa siku 12, Israel ilishambulia vituo vya kijeshi na vya nyuklia vya Iran huku Marekani ikijiunga baadaye kwa kushambulia vinu vikuu vya nyuklia.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW