1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroIran

Iran yathibitisha kifo cha afisa wa usalama Ali Larijani

18 Machi 2026

Iran imethibitisha kifo cha afisa mwandamizi wa usalama Ali Larijani, saa chache baada ya Israel kusema imemuua mkuu huyo wa usalama wa Iran katika shambulizi la anga huko Tehran.

Iran Tehran 2026 | Maandamano ya Siku ya Al-Quds pamoja na Ali Larijani mjini Tehran
Afisa mwandamizi wa usalama nchini Iran Ali Larijani ameuawa katika shambulizi la Israel nchini humoPicha: Iranian President's Press Office/UPI Photo/IMAGO

Shirika la habari la Fars, lenye mafungamano na Kikosi cha Walinzi wa Mapinduzi -IRGC- lilitangaza kuhusu kifo chake na kusema ameuawa kama "shahidi."

Larijani alihudumu kama mshauri wa karibu wa kiongozi mkuu Ayatollah Ali Khamenei, aliyeuawa katika shambulizi la anga Februari 28, siku ambayo vita vya Marekani na Israel dhidi ya Iran vilipozuka.

Tehran pia imethibitisha kifo cha kamanda wa vikosi vya usaidizi vya Basij, Brigedia Jenerali Gholam Reza Soleimani.

Shirika la habari la Fars lilichapisha taarifa ya kifo chake, ambapo Kikosi cha Walinzi wa Mapinduzi walimpongeza kwa "ushahidi wake wa heshima," huku kikisema wapiganaji wa Basij kamwe hawataacha kulipa kisasi cha kifo cha kiongozi wao.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW