1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Iran yatishia kushambulia kambi za Marekani

11 Juni 2025

Waziri wa Ulinzi wa Iran Aziz Nasirzadeh, amesema nchi hiyo itajibu mgogoro wowote utakaotokea iwapo majadiliano ya nyuklia kati ya Jamhuri hiyo ya kiislamu na Marekani yatafeli.

Aziz Nasirzadeh | Iran
Waziri wa Ulinzi wa Iran Aziz NasirzadehPicha: IRNA

Nasirzadeh amesema taifa lake litakuwa tayari kushambulia kambi za kijeshi za Marekani zilizopo katika kanda ya Mashariki ya Kati iwapo mgogoro utatokea baada ya kushindwa kufikia mkataba wa nyklia na Marekani.

Ameyasema hayo kuelekea duru ya sita ya mazungumzo hayo ya nyuklia kati ya mahasimu hao wa muda mrefu. Marekani imesema mazungumzo hayo yatafanyika siku ya Alhamisi wiki hii huku Iran ikisema mazungumzo yatafanyika siku ya Jumapili nchini Oman.

Iran yaituhumu Marekani kuhujumu mazungumzo ya Nyuklia

Rais wa Marekani Donald Trump ametoa vitisho mara kadhaa kwa Iran kuwa ataishambulia kwa mabomu iwapo hawatafikia mkataba huo wa nyuklia. 

Hata hivyo Aziz Nasirzadeh amesema hivi karibuni Iran ilifanya jaribio la makombora yake na haitakubali kamwe kudhibitiwa. Kiongozi Mkuu wa taifa hilo  Ayatollah Ali Khamenei alisema mwezi Februari kwamba Jamhuri hiyo inapaswa kuendelea kuimarisha jeshi lake ikiwa ni pamoja na makombora yake. 
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW