1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIran

Iran yawakamata 4 kwa shambulio la sumu katika shule

2 Machi 2023

Mamlaka nchini Iran imewakamata leo watu wanne wanaoshukiwa kuhusika na shambulio dhidi ya mwanamke mmoja nje ya shule ya wasichana iliyolengwa katika wimbi la mashambulizi ya kutumia sumu.

Iran Mädchenschulen Vergiftungen
Picha: irna.ir

Mamia ya visa vya matatizo ya kupumua vimeripotiwa katika muda wa miezi mitatu iliyopita miongoni mwa wasichana wa shule, katika kile afisa mmoja wa serikali anasema kinaweza kuwa jaribio la kulazimisha kufungwa kwa shule za wasichana katika jamhuri hiyo ya Kiislamu.

Siku ya Jumatano, takriban shule 10 za wasichana zililengwa na mashambulizi ya sumu, saba katika mji wa kaskazini-magharibi wa Ardabil na tatu katika mji mkuu Tehran.

Waziri wa mambo ya ndani wa Iran Ahmad Vahidi amelitaka jeshi la polisi kuanzisha mara moja uchunguzi juu ya vitendo hivyo.