UgaidiIran
Iran: Washukiwa 3 waliokuwa wakipanga mashambulizi wakamatwa
6 Aprili 2024Matangazo
Washukiwa hao waolikamatwa katika mji wa Karaj, katika jimbo la kaskazini magharibi la Alborz, ni Mohammed Zakar anayetambuliwa kama afisa mwandamizi wa kundi hilo, hii ikiwa ni kulingana na shirika la habari la Iran, IRNA.
Hata hivyo, shirika hilo halikuweka wazi mara moja, ni wapi washukiwa hao walikamatwa au kama kulikuwa na raia wa kigeni.
IRNA pia liliripoti juu ya kukamatwa kwa watu wengine wanane waliohusishwa na mpango huo, lakini hakukuwa na maelezo zaidi.
Mwezi Januari, IS walitangaza kuhusiaka na mashambulizi mawili katika jiji la kusini mwa Iran la Kerman, yaliyowaua zaidi ya watu 90.