1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Iran yawatia mbaroni viongozi wanane wa mgomo

14 Mei 2023

Vyombo vya habari nchini Iran vimeripoti kuwa mamlaka zimewatia mbaroni watu wanane kwa "kuongoza" mgomo wa wafanyakazi

Iran | Lehrerproteste
Picha: UGC

Vyombo vya habari nchini Iran vimeripoti kuwa mamlaka zimewatia mbaroni watu wanane kwa "kuongoza" mgomo wa wafanyakazi katika eneo muhimu la gesi kusini mwa nchi hiyo.Naibu gavana Akbar Pourat amenukuliwa na shirika la habari la Tasnim akisema "Viongozi wanane wakuu wa mgomo wa wafanyakazi katika miradi ya "South Pars" wamekamatwa na idara za ujasusi."Takriban watu 40,000 wameajiriwa katika kampuni za South Pars/North Dome Mega-Field, eneo ambalo linakadiriwa kuwa ni hifadhi kubwa zaidi ya gesi duniani, ambako Iran inashirikiana na Qatar katika umiliki wake.Itakumbukwa mwishoni mwa Aprili mamlaka nchini humo ilikwishatangaza kwamba imeanza kuziba nafasi ya wafanyikazi 4,000 ambao walikuwa wakigoma kudai mishahara bora na mazingira ya kufanya kazi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW