1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Iran: Zaidi ya raia 50 kurejea kutoka Marekani

7 Desemba 2025

Iran imesema leo kuwa zaidi ya raia wake 50 watarejea kutoka Marekani, katika wakati ambapo Rais Donald Trump anaendeleza msako dhidi ya wahamiaji.

Iran Teheran 2025 | Esmail Baghaei
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa Iran Esmail Baghaei katika mkutano na waandishi wa habari mjini Tehran mnamo Oktoba 13, 2025Picha: Sha Dati/Xinhua/picture alliance

Wakati wa mkutano wa kila wiki na waandishi wa habari, msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Iran Esmail Baghaei amesema katika siku zijazo, karibu raia 50 hadi 55 wa Iran watarejea nchini humo.

Baghaei amesema hilo ni kundi la pili katika miezi ya hivi karibuni kurejea Iran.

Msemaji huyo amekosoa kile alichokiita "vitendo vya kibaguzi vya Marekani dhidi ya raia wa kigeni, hasa raia wa eneo lao na hasa Wairani".

Ameongeza kuwa ni dhahiri kwamba shinikizo hizo zimechochewa kisiasa na kwamba sera hizo za kupinga uhamiaji zinakinzana na sheria za haki za binadamu.

Kwa mujibu wa CNN, kundi hilo linatarajiwa kuwasili Iran baadaye leo baada ya ndege wanayosafiria kusimamia kwa muda nchini Kuwait.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW