1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Iran,Russia,Uturuki kuweka msimamo wa pamoja Syria

Sekione Kitojo
3 Aprili 2018

Iran,Urusi na Uturuki zimejiweka pamoja kuunda nguvu ya muungano wa mataifa matatu wenye lengo la kuimarisha hatua  kujiingiza  Syria, na kuchukua fursa ya kusitasita mataifa ya magharibi kujiingiza kijeshi nchini humo.

Türkei Recep Erdogan & Wladimir Putin in Ankara
Picha: picture-alliance/Anadolu Agency/K. Ozer

Marais  wa  mataifa  hayo  matatu , Vladimir Putin , Recep  Tayyip Erdogan , na  Hassan Rouhani  wa  Iran ,  ambao  kwa  muda  mrefu walionekana  kuwa  mahasimu  wa  kimkoa  badala  ya  washirika wa  kimkakati, watakutana  leo  mjini  Ankara kwa  mkutano  wao  wa pili  wa  kilele  kuhusu  Syria  katika  hatua  ya  kuonesha  umoja wao.

Rais Vladimir Putin(kushoto) na Erdogan wa Uturuki (kulia)Picha: Reuters/Sputnik/Mikhail Klimentyev/Kremlin

Mkutano  huu , ambao  unafuatia  mkutano  wa  kwanza  wa  kilele baina  ya  viongozi  hao  mjini  Sochi Novemba  mwaka  jana, unakuja  wakati  Uturuki  ikiwania  kupata  sauti  kubwa  baada  ya kuazisha  mashambulizi  dhidi  ya  wanamgambo  wa  Kikurdi  ndani ya  Syria.

Rais  wa  Marekani  Donald  Trump ameashiria  kwamba   nchi  yake itakuwa  inajiondoa "hivi  karibuni" kutoka  Syria , katika  hatua ambay  itaimarisha  ushawishi  wa  Uturuki , Urusi  na  Iran   nchi ambazo zimekuwa  na  majeshi  yao  ndani  ya  nchi  hiyo.

Sinan Ulgen , mwenyekiti wa  kituo  cha  sra za  mchanganuo wa mawazo  katika  masuala  ya  kiuchumi  na  sera  za  mambo  ya kigeni  cha  mjini  Istanbul, amesema  mataifa  hayo  matatu sasa yamekuwa  wadhibiti  wakuu  ndani  ya  Syria.

Ulgen  aliliambia  shirika  la  habari  la  AFP  kwamba  mataifa  hayo matatu  yamekuwa  "mataifa  yenye  nguvu  kimkoa ambayo  yako tayari  kuwekeza  rasilmali za  kijeshi  kushawishi  matokeo ya mzozo  huo."

Eneo la Ghouta mashariki likiwa majengo yake yamebakia magofuPicha: Imago/Xinhua/A. Safarjalani

Mataifa  hayo  matatu  mwaka  jana  yalianzisha  mchakato wa kuleta  amani  sambamba na  mazungumzo  yanayoongozwa  na Umoja  wa  mataifa  mjini  Geneva. Mazungumzo  hayo , ambayo yanafanyika  Astana, yamefanyika  mara  kadhaa  bila  ya  kupata suluhisho.

Mchakato  wa  Astana

"Mchakato wa  mjini  Astana  ni  chombo ambacho  Uturuki , Urusi na Iran , vinakiangalia  kuweza  kudhibiti  vita  na  kupata  maslahi  yao mbali  mbali," amesema  Elizabeth Teoman , mchambuzi  wa  Uturuki katika  taasisi iliyoko  mjini  Washington  katika  mitaala  ya  vita (ISW).

Urusi ina uwezo  mkubwa  wa  nguvu  za  angani  nchini  Syria wakati  Iran ina  vikosi  vya jeshi  lake  la  ardhini , kwa  kiasi  fulani kwa  kutumia  makundi  ya  wanamgambo  ambayo  ni  pamoja  na wapiganaji  wa  kigeni.

Lakini  Erdogan ameongeza  ushawishi  wa  Uturuki  kwa  kuazisha mwezi  Januari  mashambulizi  kuukamata  ardhi  kutoka  kwa  vikosi vya  wanamgambo  wa  ulinzi  wa  umma  vya  Wakurdi  vya  YPG.

Mashambulizi  hayo  tayari  yamefanikisha  kukamatwa  kwa  eneo la  zamani  wa  YPG la  Afrin  na  Erdogan  ametishia  mara  kadhaa kuendeleza  msukumo  wake  kuelekea  zaidi upande  wa  mashariki.

"Erdogan  ni  mshirika  dhaifu  kwa  misingi  wa  majeshi  ya  ardhini na  udhibiti  wa  anga. Lakini amejenga  uwiano  na  kuthibitisha kwamba  anaweza  kujenga  uwezekano   ndani  ya  nchi  hiyo," amesema  Teoman.

Kinu cha kinyuklia cha UturukiPicha: picture-alliance/dpa/AA/N. Shvetsov

Lakini  wachambuzi  bado  wana  shaka  juu  ya  uwezekano  wa muda  mrefu  wa  utendaji  wa  muungano  huo  kati  ya  mataifa hayo  makubwa  matatu  ambayo  yametumia  historia  yao  kubwa ya  vita  na  kupigana  vikumbo  kuwania  ushawishi  katika  eneo hilo  la  bahari  nyeusi. Kinadharia  bado wanaendelea  kuwa  katika pande  zinazotofautiana  katika  mzozo  huo , ambapo  Urusi  na  Iran zikitoa  usaidizi  wa  kijeshi  kwa  utawala  wa  Syria  wa  rais Bashar al-Assad   lakini  Uturuki  mara  kwa  mara  ikitoa  wito   Assad aondolewe.

Mwandishi: Sekione  Kitojo / afpe

Mhariri: Mohammed Abdul Rahman

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW