1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroIran

Iraq yaulalamikia Umoja wa Mataifa kuhusu visa vya Israel

28 Oktoba 2024

Iraq imeandika barua ya kulalamika kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Gutteres na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, ikilaani hatua ya Israel ya kutumia anga yake kuishambulia Iran.

Iran | Tehran
Picha ikionyesha mwonekano wa Tehran, Iran, Oktoba 26, 2024. Milipuko kadhaa ilisikika katika mji mkuu wa Iran Tehran mapema Jumamosi, runinga ya serikali ya IRIB iliripoti.Picha: Yao Bing/Xinhua//picture alliance

Hayo yameelezwa leo na serikali ya mjini Baghadad kupitia msemaji wake Bassim Alawadi.

Amelaani kile alichokiita, ukiukaji wa wazi wa Wazayuni, wa anga na mamlaka ya Iraq kwa kufanya shambulizi dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu yaIranmnamo Oktoba 26.

Kwa upande mwingine kamanda mwandamizi wa jeshi la ulinzi wa mapinduzi ya Iran, Hossein Salami  ameionya Israel, akisema itakabiliwa na hatua kali baada ya shambulizi lililoyalenga maeneo ya kijeshi ya Iran.

Kamanda huyo amesema Israel ilishindwa kufikia malengo yake kupitia mashambulizi hayo ya anga.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW