Iraq, Misri na Jordan zafanya mkutano wa kilele
28 Juni 2021Rais Abdel Fattah al-Sisi na Mfalme Abdullah wa Pili wa Jordan wamekutana na Rais wa Iraq Barham Saleh pamoja na Waziri Mkuu Mustafa al-Kadhemi ambapo rais Saleh anasema mkutano huo ulikuwa na maana kubwa katika eneo hilo linalokabiliwa na changamoto nyingi.
Ziara hiyo ya Rais al-Sisi na Mfalme Abdullah inafanyika katika kipindi ambacho Iraq inafanya jitihada za kujisogeza karibu na mataifa ya kiarabu ambayo ni washirika wa Marekani katika eneo la Mashariki ya Kati.
Iraq ipo katika jitihada ya kuwa msuluhishi wa migogoro ya kikanda.
Iraq vilevile ipo katika jitihada ya kujipa fursa ya upatanishi miongoni mwa mataifa ya Kiarabu na Iran, baada ya kuripotiwa kuwa mwenyeji wa mazungumzo ya serikali za Tehran na Riyadh ya April. Akizungumza katika hitimosho la mkutano huo Waziri Mkuu wa Iraq aliosema pamoja na mengine sio siri kwa wakati huu adui mkubwa wa ulimwengu ni janga la Covid 19 pamoja na vita dhidi ya ugaidi. Aidha alongeza.
Kadhimi al Kadhimi aliongezea zaidi "Kama tulivyokubaliana katika siku za nyuma, tutaendelea kushirikiana katika maeneo kadhaa ya kikanda kama Syria, Libya, Yemen pamoja na Palestina, na kuweka mkazo wa pamoja katika ushirikiano na uratibu kuhusu mataifa hayo kwa lengo la kuwafanya ndugu zetu wa mataifa hayo kuvuka kiunzi cha nchangamoto hizo."
Mgogoro wa Syria umepewa mtazamo wa kipekee.
Kwa zingatio la vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Syria, ambavyo vimedumu kwa miaka 10 sasa viongozi hao kwa zingatio la maazimo ya Umoja wa Mataifa wamejadili suala la usalama na kuandaliwa mazingira bora ya kurejesa kwa wakimbizi waishio uhamishoni.
Uhusiano baina ya Iraq na Misri umezidi kuwa bora katika siku za hivi karibuni ambapo maafisa baina ya mataifa hayo mawili wamekuwa wakifanya ziara za kutembeleana za mara kwa mara. Na al Sisi anakuwa rais wa kwanza kuwasiliBaghdad tangu aliyekuwa rais wa taifa hilo Sadam Hussein kuivamiwa Kuwait 1990. Lakini Mfalme wa Jordan aliwasili nchini humo mapema 2019 kwa mara ya kwanza baada ya miaka 10.
Hivi karibuni vyombo vya habari viliibua habari za serikali ya Saudia Arabia na Iran zilikutana April, ukiwa mkutano wao mkubwa wa ngazi za juu, tangu serikali ya Saudia ikatishe uhusiano wake na serikali ya Iran 2016.
Chanzo: AFP