1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Iraq na Kuwait zaingia kwenye mvutano wa mpaka wa baharini

23 Februari 2026

Mataifa ya kiarabu ya ghuba majirani wa Kuwait yameiunga mkono nchi hiyo katika mvutano wake wa mpaka wa baharini na Iraq

Majirani wa Kuwait,Uae, Qatar, Oman zaiunga mkono Kuwait kwenye mvutano wake na Iraq kuhusu mpaka wa bahari kwenye ghuba ya uajemi
Majirani wa Kuwait,Uae, Qatar, Oman zaiunga mkono Kuwait kwenye mvutano wake na Iraq kuhusu mpaka wa bahari kwenye ghuba ya uajemiPicha: NASA Earth/ZUMA Press/picture alliance

Mvutano kuhusu mpaka wa baharini kati ya Iraq na Kuwait ulioibuka mwishoni mwa juma umeyachochea mataifa ya kiarabu ya eneo la Ghuba kuiunga mkono Kuwait, na kuiacha Baghadad ikitowa malalamiko yake.

Mvutano huo umeibuka baada ya hivi karibuni Iraq kuwasilisha ramani na ushahidi wa kijiografia mbele ya Umoja wa Mataifa ikidai baadhi ya maeneo kwenye bahari ya ghuba ya Uajemi yako chini ya himaya yake.

Maeneo hayo ambayo ni pamoja na Fasht al-Qaid na Fasht al-Aij, kimsingi Kuwait imekuwa ikidai yako kwenye nchi yake. Qatar,Umoja wa Falme za kiarabu na Oman ambazo ni majirani wa Kuwait zimetowa matamko ya kuonesha mshikamano na nchi hiyo.

 Pamoja na kwamba mahusiano kati ya Iraq na Kuwait yameimarika tangu alipoondolewa Saddam Hussein mwaka 2003 aliyeivamia Kuwait mwaka 1990, suala la mipaka ya baharini limekuwa mara zote likizusha mivutano baina ya mataifa hayo mawili.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW