1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUswidi

Iraq yamfukuza balozi wa Sweden

20 Julai 2023

Serikali ya Iraq imemtaka Balozi wa Sweden mjini Baghdad kuondoka mara moja katika ardhi ya nchi hiyo na kuamuru mwanadiplomasia wake kuondoka nchini Sweden.

Themenpaket | Irak Protest Botschaft Schweden
Picha: AHMED SAAD/REUTERS

Uamuzi huu umechukuliwa baada ya Iraq kuifahamisha Sweden kuwa ingelivunja mahusiano ya kidiplomasia ikiwa Qur'an itachomwa tena moto mjini Stockholm baadaye leo.

Taarifa zinabaini kuwa waandamanaji mjini Stockolm hii leo wameharibu na kukidhalilisha kwa kukikanyaga kitabu kitakatifu cha Qur'an lakini hawakukichoma moto kama walivyokuwa wametishia hapo awali.

Haya yanajiri pia baada ya usiku wa jana, mamia ya waaandamanaji kuvamia na kuuchoma moto Ubalozi wa Sweden mjini Baghdad, kitendo kilicholaaniwa vikali na serikali ya Sweden.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW