1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JangaIraq

Iraq yaomboleza vifo vya mkasa wa moto

27 Septemba 2023

Iraq inaomboleza vifo vya karibu watu 100 waliopoteza maisha kwa mkasa wa moto uliozuka kwenye ukumbi wa harusi kaskazini mwa nchi hiyo usiku wa kuamkia leo.

Mabaki ya ukumbi uliotetekea kwa moto Iraq
Mabaki ya ukumbi uliotetekea kwa moto IraqPicha: Abdullah Rashid/REUTERS

Moto huo ambao chanzo chake bado hakijafahamika, ulizuka ndani ya ukumbi uliofurika watu waliohudhuria harusi ya wanandoa kutoka jamii ya wakristo wachache wa Iraq. 

Mamlaka za nchi hiyo zinasema zaidi ya watu wengine 150 wamejeruhiwa kwenye mkasa huo wa kuhuzunisha uliotokea kwenye  wilaya ya Hamdaniya, kiasi kilometa 335 kutoka mji mkuu, Baghdad.

Soma pia:Iraq yalaani mashambulizi ya Uturuki

Wengi ya waliojeruhiwa na moto huo ambao unadhaniwa huenda ulisababishwa na fashi fashi zilizorushwa ukumbini, wanapatiwa matibabu katika hospitali kadhaa za jimbo la Neneveh, kaskazini mwa nchi hiyo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW