1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Iraq yatarajia Trump atatimiza ahadi ya kusitisha vita

9 Novemba 2024

Iraq imeelezea matumaini yake kwamba utawala mpya wa Rais Donald Trump wa Marekani unaoanza kazi Januari 2025 utaweka msisitizo kwenye kutekeleza ahadi ya kusimamisha vita na sio kuanzisha vita vyengine ulimwenguni.

Iraq Mohammed Shia Al-Sudani
Waziri Mkuu wa Sudan, Mohammed Shia al-SudaniPicha: Murtadha Al-Sudani/Anadolu Agency/Pool via REUTERS

Waziri Mkuu wa Iraq, Mohammed Shia al-Sudani, ameyaelezea matumaini yake wakati wa mazungumzo yake kwa njia ya simu na rais mteule wa Marekani, Donald Trump, kwamba atatimiza ahadi yake kufanya kazi kuelekea kusitisha vita vya Mashariki ya Kati.

Sudan amekuwa akiweka juhudi kubwa kuhakikisha nchi yake haiburuzwi katika vita hivyo. 

Soma zaidi: Iraq imelaani matumizi ya Israel ya anga yake kushambulia nchi jirani ya Iran

Kwenye mazungumzo yake alimkumbusha Trump kuhusu taarifa na ahadi zake za kumaliza mzozo wa kanda hiyo, na pande hizo mbili zimekubaliana kuunganisha juhudi hizo ili kufanikisha malengo ambayo ni kuvimaliza vita na kurejesha amani ya Mashariki ya Kati.

Wanajeshi wa Marekani 2,500 wapo nchini Iraq kama sehemu muungano unaoongozwa na Marekani ulioundwa kusaidi kupambana na kundi lijiitalo Dola la Kiislamu (IS).

Soma zaidi: Israel yafanya mashambulizi ya anga dhidi ya Iran

Makambi ya wanajeshi hayo yamekuwa wakilengwa kwa maroketi na droni kutoka kwa makundi yanayoungwa mkono na Iran ambayo pia yamekiri kufanya mashambulizi dhidi ya Israel kupinga vita Israel inavyoviendeleza kwa wapalestina katika Ukanda wa Gaza.