1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Iraq yatumbukia kwenye mgawanyiko

27 Desemba 2019

Raia wa Iraq wamegawika juu ya kitisho cha kujiuzulu rais wa nchi hiyo anayepinga kuidhinisha jina la waziri mkuu anayeungwa mkono na makundi yanayoegemea Iran.

Porträts von Frontlinien globaler Proteste
Picha: Reuters/T. al-Sudani

Baadhi wameitaja hatua hiyo ya rais kuwa kinyume na katiba lakini wengine wamemsifu kwa kutimiza wajibu wake kama kiongozi wa nchi. 

Rais Barham Saleh wa Iraq amekataa majaribio yote ya muungano wa wabunge wanaoegemea Iran ya kupendekeza wagombea wadhifa wa uwaziri mkuu akiwemo waziri aliyezulu na gavana aliye na rikodi tata.

Hapo jana Saleh alisema yuko tayari kujiuzulu kuliko kumuidhinisha Asaad al-Eidani  mgombea ambaye tayari amekataliwa na vuguvugu la  maandmanao ya umma lililofanikiwa kuiangusha serikali iliyopita.

Waaandamanaji wamesema wanataka waziri mkuu huru asiye na mafungamno na tawala lililo madarakani hivi sasa 

Kiasi watu 460 wameuwa na wengine zaidi ya 25,000 wamejeruhiwa tangu kuzuka wimbi la maandamano mnamo mwezi Oktoba kudai mageuzi mapana ya kisiasa na ambayo hadi sasa hayana ishara ya kupungua nguvu.

Al Sistani ajitenga kuzungumzia siasa Ijumaa ya wiki hii

Kiongozi wa kidini nchini iraq, Ali al-SistaniPicha: Imago Images/Zuma

Wakati taifa hilo likiwa limetumbukia kwenye mzozo wengi walitumai ujumbe wa kila wiki wa kiongozi wa kidini aliye na ushawishi mkubwa Ayatollah Ali Sistani ungetoa mwelekeo wa kile kitakachofuata lakini kiongozi huyo hakuzungumzia chochote leo kuhusu hali ya kisasa nchini Iraq.

Katika uwanja wa Tahrir mjini Baghdad, ambao ndiyo kitovu cha vuguvgu la maandamano bango waandmanaji walitundika bango kubwa lenye picha za wagombea waliokataliwa kwa wadhifa wa waziri mkuu huku sura zikichorwa alama ya X yenye rangi nyekundu.

"Shukran Barham kwa kuegemea upande wa matakwa ya umma na kuwakataa wagombea wa vyama vilivyojaa rushwa, Tuko pamoja na wewe" linasomeka bango hilo

Lakini siyo waandamanaji wote wanakubaliana na fikra hiyo, wengine wamesema kujiuzlu kwa rais Saleh kutawezesha kuvunjwa wka bunge na kufanyika uchaguzi na mapewa utakaowapa nafasi wapiga kura ya kuwaondoa madarkaani wanasiasa wote w´laghai na wala rushwa.

Migawanyiko imeshuhudiwa pia hata katika tabaka tawala .

Rais Barham Saleh wa IraqPicha: picture-alliance/AP Photo/K. Kadim

Kundi linalounga mkono Iran linadai ambalo ndiyo kubwa ndani ya bunge na lenye haki ya kupendekeza jina la waziri mkuu wametaka wabunge wachukue hatua za kisheria dhidi ya rais Saleh kwa kuvunja masharti ya katiba.

Lakini kundi la waziri mkuu wa zamani Haider al-Abadi ambalo sasa liko upande wa upinzani limemrai rais Saleh kutafakari upya nia yake ya kujiuzulu na badala yake afanye kazi kwa pamoja na pande zote ili kuleta mabadiliko katika utawala wa nchi hiyo.

Kundi hilo la Abadi ambalo lilishika nafasi ya tatu katika uchaguzi uliopita limesema makundi kinzani sharti yanaondoe fikra ya vitisho, hujuma na kutaka kuchukua udhibiti kwa kuwa hali hiyo inatishia kuitumbukiza Iraq katika hali mbaya zaidi.

Mkwamo unaondelea nchini humo umeiweka kambi ya wanaoegemea Iraq kwenye mvutano dhdii ya waandamanaji waliopania kupata na wanachotaka ambao hadi sasa wamefanikiwa kufungwa kwa shule na ofisi za umma katika eneo la kusini.

Waandamanaji wamesema vurugu zitaendelea hadi matakwa yote yatakapotekelezwa kikamilifu.

Waandamanaji wanataka kufumuliwa kwa mfumo mzima wa utawala unaogawa madaraka kwa upendeleo wa kikabila na madhehebu na wanataka kujiuzulu kwa tabaka tawala ambalo liko madarakani kwa miaak 16.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW