1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSyria

Iraq yawarejesha makwao wakimbizi 625 kutoka kambi ya Syria

11 Machi 2024

Takriban familia 160 za Wairaq zimerejeshwa kutoka kambi ya Al-Hol Syria, makazi ya maelfu ya watu wakiwemo wanaoshukiwa kuwa wenye itikadi kali. Taarifa hiyo imetolewa jana Jumapili na msemaji wa serikali ya Iraq.

Syrien Camp Roj
Wanawake na watoto wanatembea kwenye kambi ambapo jamaa za watu wanaoshukiwa kuwa wa kundi la Dola la kiislamu wanashikiliwa kaskazini mashariki mwa Syria, Machi 28, 2021Picha: Delil Souleiman/AFP/Getty Images

Msemaji wa Wizara ya Uhamiaji ya Iraq, Ali Abbas aliliambia Shirika la Habari la Ufaransa  AFP kwamba kambi ya Al-Hol inawahifadhi jamaa za watu wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa kundi la Dola la Kiislamu pamoja na wakimbizi.

Amesema familia 157, au jumla ya watu 625 wamerejea Iraq kutoka Al-Hol siku ya Jumamosi katika juhudi za hivi karibuni za kuwarejesha makwao.

Zaidi ya Wasyria 43,000, Wairaq na wageni kutoka nchi zisizopungua 45 wanaishi katika kambi hiyo yenye hali ngumu na iliyojaa watu wengi kaskazini mashariki mwa Syria inayodhibitiwa na Wakurdi.