1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Iraq yawasaka walioiba $2.5 billioni

4 Machi 2023

Mahakama nchini Iraq imetoa waranti wa kukamatwa maafisa wanne wa zamani wanaotuhumiwa kwa kuwezesha wizi wa fedha za umma zenye thamani ya dola bilioni 2.5.

Irak Premierminister Mustafa al-Kadhemi
Picha: Ludovic Marin/abaca/picture alliance

Taarifa hiyo ilitolewa siku ya Jumamosi (Machi 4) na mamlaka ya kupambana na ufisadi nchini Iraq ambayo imeutaja wizi huo kama moja ya kashfa kubwa zaidi za ufisadi kuwahi kutokea nchini humo.

Afisa mmoja wa katika mamlaka hiyo, ambaye hakutaka kutajwa jina, alisema watu hao ni pamoja na waziri wa zamani wa fedha na ndugu wa waziri mkuu wa zamani, Mustafa al-Kadhemi, ambaye anaishi nje ya nchi.

Soma zaidi: Wafuasi wa Sadr waondoka majengo ya serikali
Kundi la ulamaa mwenye usemi mkubwa Iraq al Sadr latwaa ushindi

Kwa mujibu wa afisa huyo, watu hao ni waziri wa zamani wa fedha, Ali Allawi, aliyekuwa mkurugenzi wa baraza la mawaziri, Raed Jouhi, katibu wake, Ahmed Najati, pamoja na mshauri wake, Mushikir Abbas.

Fedha hizo ziliibwa kati ya Septemba 2021 na Agosti 2022.