1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ireland na Jamhuri ya Czech zapiga kura uchaguzi wa EU

7 Juni 2024

Wapiga kura katika nchi za Umoja wa Ulaya za Ireland na Jamhuri ya Czech wataanza leo mchakato wa kupiga kura ulioingia siku yake ya pili kwenye nchi za Umoja huo baada ya Uholanzi kufungua mchakato huo.

Nchini Uholanzi chama cha siasa kali za mrengo wa kulia cha Freedom Party PVV kinachopinga uhamiaji na chenye mashaka na Umoja wa Ulaya, kinajiandaa kupata nguvu kubwa katika bunge la Umoja wa Ulaya baada ya matokeo ya awali kuonesha kinashikilia nafasi ya pili kikiwa na viti saba. 

Hatua hiyo inatarajiwa kuwa ya kwanza katika msururu wa mafanikio ya vyama vya siasa kali vya mrengo wa kulia kote katika Umoja wa Ulaya.

Soma pia:Uchaguzi wa bunge la Ulaya waanza Uholanzi

Utafiti unaonesha vyama hivyo vinaweza kuzowa  robo ya viti vyote 720 vinavyowaniwa. 

Nchi nyingi kati ya 27 za Umoja huo ikiwemo Ujerumani na Ufaransa zitapiga kura Jumapili.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW