1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

IRKUTSK: Ndege ya abiria yapata ajali Siberia

9 Julai 2006

Watu wasiopungua 118 wamefariki katika ajali ya ndege iliyotokea katika mji wa Irkutsk mashariki mwa Siberia.Ripoti zasema wengine 53 walijeruhiwa na wamepelekwa hospitali.Ndege hiyo aina ya Airbus 310 ilipotua uwanjani,ilishindwa kusimama na ikagonga ukuta na kushika moto.Katika ndege hiyo ya Sibir Airlines ilikuwa na watu 200,ikiwa ni pamoja na wahudumu wa ndege.Idadi kubwa ya abiria walikuwa watu waliotaka kwenda likizoni kwenye Ziwa Baikal.Miongoni mwao walikuwepo watoto vile vile.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW