IS walipataje silaha zao nchini Iraq na Syria ?
2 Machi 2018Hususan wakaazi wa maeneo hayo yaliyokombolewa waliathirika kwa kiasi kikubwa. Watu 10,000 waliuwawa. Mji mkuu wa kundi hilo la IS Rakka nchini Syria ni magofu matupu, kama ulivyo mji wa Mosul, Ramadi ama Tikrit nchini Iraq.
Hali iliyochukua muda mrefu kwa IS kuwapo katika maeneo hayo na udhibiti wao kuulinda kwa kumwaga damu, hauhusiani tu na itikadi kali ya wafuasi wake. Muhimu kabisa ilikuwa hali ya kuendelea kwa upatikanaji wa silaha kwa wapiganaji hao wa Jihadi.
Sehemu kubwa ya silaha hizi zinatoka katika mataifa wanachama wa NATO barani Ulaya na Umoja wa Ulaya, kupitia Marekani na Saudi Arabia. Hii imeelezwa na shirika la kimataifa la utafiti wa silaha katika maeneo yenye mizozo, katika utafiti uliofanywa kwa miaka mitatu.
Watafiti wa shirika hilo walikuwa katika maeneo ya mapigano kati ya julai 2014 na Novemba 2017.
Walishuhudia silaha na vifaa vya kivita , ambavyo wapiganaji wa muungano unaopambana na kundi la IS walikuwa nazo. Kati ya Kobane na mpaka kati ya Syria na Uturuki pamoja na mji mkuu wa Iraq Baghdad, wataalamu wa shirika hilo walionesha kiasi ya silaha 2000 na zaidi ya risasi 40,000. Na waliweza kuonesha ushahidi wa namba za silaha hizo na njia zilizopitia hadi kuwafikia wapiganaji hao wa IS. Nani aligharamia, kazi hiyo ilifanywa na Umoja wa Ulaya na wizara ya mambo ya kigeni ya Ujerumani.
Inashangaza
Damian Spleeters ni mkuu wa operesheni wa shirika hilo la CAR nchini Syria na Iraq na kiongozi mkuu wa ripoti iliyotokana na utafiti huo. Katika mahojiano na shirika la utangazaji la DW Spleeter amefafanua , kile ambacho kilimshangaza zaidi.
"Kitu kilichonishangaza sana ni kwa namna gani baadhi ya silaha zimeweza kuwafikia IS kwa haraka hivyo, mara tu baada ya kuuzwa. Tuna ripoti inayozungumzia baadhi ya silaha ambazo zimesafirishwa kuanzia katikati ya Disemba 2016 na zilikuwa zinatumiwa na IS nchini Iraq, chini ya miezi mitatu baada ya kuuzwa".
Kama mfano Spleeters anataja kombora la kupambana na vifaru lililotengenezwa nchini Bulgaria. Kombora hilo liliuzwa nchini Marekani Disemba 2015, na miezi miwili baadaye baada ya majeshi ya Iraq kuukomboa mji wa Ramadi kombora hilo lilipatikana baada ya wapiganaji wa IS kuliacha wakati wanakimbia.
haifahamika wazi iwapo kombora hilo lilipatikana katika mapambano na IS , ama liliachwa na wapiganaji waliokimbia ama walilinunua kutoka katika makundi yanayopigana, hilo bado halijulikani. Bulgaria ilithibitisha kwamba kombora hilo liliuzwa nchini Marekani. Komora hilo la kupambana na vifaru liliuzwa kwa kampuni ya Marekani ya Kiesler inayonunua silaha kwa ajili ya jeshi la polisi la Marekani. Marekani hata hivyo inasema haihusiki. Silaha hizo hata hivyo zinafika katika eneo la Mashariki ya Kati.
Mtaalamu wa shirika hilo la CAR Spleeters ameona nyaraka ambazo ni muhimu sana, kwamba Saudi Arabia na Marekani ambazo ni wanunuzi wakubwa wa silaha kutoka Ulaya , hawaheshimu misingi ya Umoja wa Ulaya ya uuzaji nje silaha. Na ndio sababu hakuna ufafanuzi juu ya silaha hizo.
Hata hivyo huo ni nusu tu ya ukweli Patrick Wilken ana hakika kwamba mlolongo huo wa wauzaji unafahamu bila shaka nani anahusika, kwamba silaha hizo licha ya kuwa na nyaraka halisi zilikuwa zinaelekea katika eneo hilo la vita la Iraq na Syria. Mtaalamu huyo wa udhibiti wa silaha wa shirika la Amnesty International ameiambia DW ingekuwa kitu cha ajabu iwapo mataifa yanayohusika yasingefahamu silaha hizo zinaelekea wapi.
Mwandishi: von Hein, Matthias /ZR/ Sekione Kitojo
Mhariri: Grace Patricia Kabogo