1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

IS yakiri kuwaua wanajeshi zaidi ya 70 Burkina Faso

25 Februari 2023

Kundi la wanamgambo wa Dola la Kiislamu limekiri kuwaua zaidi ya wanajeshi 70, kuwajeruhi wengine wengi na kuwachukua mateka wanajeshi 5 baada ya kushambulia msururu wa magari ya kijeshi Kaskazini mwa Burkina Faso.

Burkina Faso | Soldaten in Kaya
Picha: Sophie Garcia/AP Photo/picture alliance

Taarifa iliyotumwa na shirika la habari la Amaq la kundi hilo, imesema lilishambulia magari ya wanajeshi yaliokuwa yakielekea katika maeneo wanayoyadhibiti karibu na eneo la Deou, lililoko katika mkoa wa Sahel wa  Oudalan.  

Kundi hilo limesema limechukua silaha za wanajeshi walioshambuliwa na kuwafurusha wengine katika maeneo ya vichakani. 

Wanajeshi 50 wa Burkina Faso wauwawa kwenye shambulizi la kustukiza

Vurugu zinazohusishwa na kundi linalofungamanishwa na kundi la kigaidi la Al Qaida, la dola la kiislamu limekuwa likiihangaisha nchi hiyo kwa miaka kadhaa na kusababisha mauaji ya maelfu ya watu huku wengine zaidi ya milioni 2 wakipoteza makaazi yao. 

Hasira ya serikali kutoweza kudhibiti hali kumepelekea jeshi kuipundua mara mbili serikali mwaka uliopita. 
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW