ISFAHAN: Iran haitoachana na mradi wa nyuklia
25 Mei 2007Matangazo
Rais Mahmoud Ahmedinejad wa Iran amesema,shughuli za kinyuklia za nchi yake zinakaribia kufikia kileleni.Akihotubia mkutano wa hadhara,katika mji wa Isfahan ulio katikati nchini Iran,Ahmedinejad alisema,serikali kamwe haitoachilia mbali harakati zake za nyuklia kwa sababu ya kushinikizwa na mataifa ya magharibi.Ametamka hayo baada ya mkuu wa shirika la kimataifa la nishati ya nyuklia,Mohamed El Baradei kusema kuwa baada ya kati ya miaka mitatu hadi mitano,Iran itakuwa na