1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ISLAMABAD. Bibi Condoleeza Rice aendelea na ziara yake Asia.

17 Machi 2005

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani bibi Condoleeza Rice ameisifu Pakistan kwa juhudi zake dhidi ya kupambana na ugaidi.

Bibi Rice ambaye yumo katika ziara ya nchi za Asia alikutana na rais wa Pakistan Parves Musharaf na waziri wake wa mambo ya nje Shaukat Aziz mjini Islamabad.

Pakistan ndio mkondo wa pili wa ziara ya bibi Condoleeza Rice ya kuzuru nchi sita za Asia kwa mara ya kwanza tangu achukue hatamu za uwaziri wa nchi za nje wa Marekani, ambako alianzia India hapo jana.

Aliusifu ushirikiano wa pakistan na India na kuendelea kwa amani baina ya nchi hizi jirani na akaongeza kusema kuwa Marekani ni mshirika wa nchi hizi mbili. India na Pakistani zote zina mipango ya kununua ndege za kivita aina ya F-16 kutoka Washington.

Bibi Condoleeza Rice pia alimueleza rais Parves Mushraf kuwa Marekani inaniunga mkono Pakistani katika kuhakikisha kufanyika kwa uchaguzi huru na wa haki nchini humo mwaka 2007.