1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ISLAMABAD: Mkutano wa viongozi wakuu wa Jumuia ya ushirikiano kusini mwa Asia wamalizika

6 Januari 2004
Mkutano wa viongozi wakuu wa nchi wanachama wa Jumuia ya ushirikiano wa mataifa ya kusini mwa bara la Asia, umemalizika leo hii katika mji mkuu wa Pakistan-Islamabad.
Tangazo la kumalizia mkutano huo, linasema mawaziri wa mambo ya kigeni wa nchi wanachama, wamesaini makubaliano ya kuanzishwa soko huru miongoni mwa mataifa ya Jumuia hiyo. Makubaliano hayo yataanza kutekelezwa kuanzia mwaka wa 2006.
Kwa mujibu wa tangazo hilo, nchi tatu zilizoendelea kiviwanda na kiuchumi kuliko nyingine za Jumuia ya ushirikiano katika eneo la Asia ya kusini, Pakistan, India na Sri-Lanka, zimekubali kuwa zitapunguza viwango vya ushuru wa bidhaa zinazoagizwa kutoka nchi hizo, au bidhaa zinazonunuliwa na wafanyabiashara wa nchi hizo kutoka nchi za Jumuia ya ushirikiano katika eneo la Asia ya kusini, kwa kiwango cha asilimia kati ya sifuri na tano. Nchi nyingine ambazo bado uchumi wake una matatizo, kama vile Bangladesh, Nepal, na nyingine, zitapewa muda wa kujiandaa kuponguza viwango vya ushuru, hadi ifikapo mwaka wa 20010.