1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Islamabad. Pakistan yatangaza hatua mpya za kupambana na uenezaji wa chuki dhidi ya watu wa dini nyingine

22 Julai 2005

.

Rais wa Pakistan Perves Musharraf ametangaza hatua mpya zinazolenga katika kuzuwia viongozi wa kidini kueneza chuki dhidi ya watu wasio Waislamu.

Akizungumzia kuhusu mashambulizi dhidi ya mji wa London , Musharraf ameahidi kushirikiana na juhudi za kimataifa za kupambana na ugaidi, lakini ametahadharisha dhidi ya kuilaumu Pakistan.

Amesema sheria hizo mpya zitalenga shule za kidini, ambazo zimekuwa shabaha ya uchunguzi wa nchi hiyo baada ya kuonekana kuwa watatu kati ya watu waliojitoa mhanga katika mashambulizi ya mabomu hapo Julai 7 mjini London walitembelea Pakistan.

Musharraf ameongeza kuwa juhudi zake hizo pia zitasitisha usambazaji wa maelezo ya chuki kupitia vyombo vyote vya habari.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW