ISLAMABAD : Wabunge wamchaguwa rais leo
6 Oktoba 2007Rais Generali Pervez Musharraf anatagemewa kushinda kipindi kengine cha miaka mitano madarakani juu ya kwamba bado hakuna uhakika iwapo Mahkama Kuu itaidhinisha uamuzi huo kwa vile mshindi hatotangazwa hadi hapo mahkama hiyo itakapotowa hukumu iwapo Musharraf anaweza kushika madaraka wakati bado akiwa kiongozi wa kijeshi.
Musharraf ameahidi kun’gatuka jeshini iwapo atachaguliwa tena na kuapishwa kushika wadhifa wa urais akiwa kiongozi wa kiraia miaka minane baada ya kuingia madarakani kwa mapinduzi. Zaidi ya wabunge 180 wa muungano wa upinzani unaoongozwa na Nawaz Sharif wamejiuzulu kupinga uchaguzi huo.
Chama cha Wananchi wa Pakistan PPP hakitosusia uchaguzi huu kufuatia Musharraf kufuta mashtaka ya rushwa dhidi ya kiongozi wake Benazir Bhutto kutokana na makubaliano ya kushirikiana madaraka.