1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ISLAMABAD:aachiwa bila ya mashtaka baada ya mahabusu ya miaka mitatu

21 Agosti 2007

Pakistan imemwachia bila ya mashtaka mtaalamu wa kompyuta alietuhumiwa kuwa na uhusiano na mtandao wa kigaidi wa al-Kaida, baada ya kumweka mahabusu kwa muda wa miaka mitatu. Mtaalamu huyo Mohammed Noor Khan alidaiwa kuwa kiunganishi baina ya viongozi wa al-Kaida na wapiganaji wa mtandao huo.