Islambrotherhood-Saddam
30 Desemba 2006Matangazo
CAIRO:
Chama cha udugu wa kiislamu nchini Misri-Muslim Bortherhood- kimelaani kunyongwa kwa rais huyo wa zamani wa Iraq Saddam Hussein katika siku kuu ya Idd-Lhaj.Kimeeleza kuchagua siku hii ya Idd kumnyonga Saddam si-ubinadamu.Kwani ,kimesema, desturi zote zinasema siku ya leo ni siku ya kusameheana.
Waislamu kote ulimwenguni wanasherehekea siku hii yenye kukumbusha mtume Ibrahim –kwa muujibu wa Qoran,alikaribua kumtoa mhanga mwanawe- Ismail pale Mungu badala yake alipompelekea kondoo kuchinja badala yake.