Israel bado inaendeleza mashambulizi yake Gaza
12 Septemba 2025
Matangazo
Mji huo ni makaazi ya wapalestina wengi waliojihifadhi huko licha ya amri ya serikali ya Israel ya kuwataka waondoke. Israel imetangaza nia yake ya kuudhibiti kikamilifu mji huo unaowahifadhi wapalestina takriban milioni moja.
Israel imesema itaendelea na mpango wake hadi pale wanamgambo wa Hamas watakapo sambaratishwa.
Walioshuhudia wanasema nyumba 15 ndani ya kambi kubwa ya wakimbizi, zililengwa kwa mashambulizi hayo ya angani.
Amjad Al-Shawa, kiongozi wa mtandao wa shirika lisilo la kiserikali la Palestina linalofanya kazi na Umoja wa Mataifa na makundi mengine ya kimataifa limesema asilimia 10 ya watu wa Gaza City wameuhama mji huo tangu Israel ilipotangaza mpango wake wa kuchukua udhibiti wa mji huo mwenzi mmoja uliopita.