1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel-Gaza zatakiwa kuongeza muda wa kusimamisha mapigano

29 Novemba 2023

Wapatanishi wa kimataifa wanaendelea kufanya juhudi za kupatikana makubaliano yatakayowezesha kuongezwa muda wa kusimamisha mapigano kati ya Israel na wanamgambo wa Hamas.

Israel | Baba akimlaki mwanae ambae alikuwa akishikiliwa na Hamas
Baba akimlaki mwanae ambae alikuwa akishikiliwa na HamasPicha: Israel Defense Forces/REUTERS

Makumi ya mateka waliokuwa wanashikiliwa na Hamas katika Ukanda wa Gaza wameachiwa na wanaendelea kuachiwa hatua ambayo Israel imesema itadumisha mapatano hayo ya kusitisha mapigano iwapo kundi la Hamas ambalo Israel, Marekani, Umoja wa Ulaya na mataifa mengine kadhaa ya Magharibi yameliorodhesha kuwa la kigaidi, litaendelea kuwaachia huru mateka na kwa upande wa Israel imesema itaendelea kuwatoa wapalestina walio fungwa kwenye jela zake.

Wakati huo huo, mawaziri wa mambo ya nje wa kundi la mataifa saba yaliyoendelea zaidi kiuchumi duniani, G7 wametoa wito wa kuachiliwa mara moja bila masharti mateka wote wanaozuiliwa katika Ukanda wa Gaza.

Katika taarifa yao, kundi hilo la mataifa yaliyoendelea kiviwanda limesema linapongeza kuachiliwa kwa baadhi ya mateka waliochukuliwa na kundi la Hamas pamoja na mashirika mengine ya kigaidi mnamo Oktoba 7.

Soma: Israel na Hamas waendelea kubadilishana mateka na wafungwa

Wanachama hao wa G7 pia wamepongeza hatua za hivi karibuni za kusitisha mapigano hali imayoruhusu kupelekwa misaada zaidi kwa wapalestina huko Gaza.

Misaada imewafikia Wapalestina

Mkurugenzi wa Shirika la Chakula Duniani WFP, Samer Abdeliaber amesema WFP imefanikiwa kufikisha misaada kwa Wapalestina wakati wa kipindi hiki cha kusimamishwa mapigano.

Lori lililobeba misaada ya kiutu likiingia katika Ukanda wa GazaPicha: Hatem Ali/AP/picture alliance

Samerameongeza kusema kuwa katika siku nne za kipindi cha kusitishwa mapigano, WFP na washirika wake wamewasilisha misaada muhimu inayohitajika kwa maelfu ya Wapalestina hata katika maeneo ambayo yalikuwa vigumu kufikiwa. 

Amesema WFP inatarajia kurefushwa kwa muda wa kusitisha mapigano hali ambayo inaweza kuwa ni fursa ya kufungua njia ya kupatikana utulivu wa muda mrefu.

Soma:Mataifa yataka kurefushwa usitishwaji mapigano Gaza 

Makubaliano ya kusimamisha mapigano kati ya Israel na Hamas yanaingia siku yake ya sita leo Jumatano. Wapatanishi wanashinikiza makubaliano endelevu kwa ajili ya kusitisha mapigano.

Baada ya makubaliano hayo kuongezwa kwa muda wa saa 48, mateka wengine 12 waliachiliwa kutoka Gaza hapo jana Jumanne, huku Wapalestina 30 wakiachiliwa kutoka kwenye jela za Israel.

Huku zikiwa zimesalia saa kadhaa kabla ya muda wa makubaliano ya kusitisha mapigano kumalizika, wapatanishi wa kimataifa wanaendelea kushughulika ili muda uongezwe na kutoa nafasi ya mateka zaidi wanaoshikiliwa na wanamgambo wa Hamas waweze kuachiliwa na pia Wapalestina waliofungwa jela nchini Israel nao waweze kuachiliwa.

Makubaliano ya kusitisha vita Israel-Hamas kurefushwa?

02:12

This browser does not support the video element.

 

 

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW