1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yaapa kujibu shambulizi la Iran la mwishoni mwa juma

Hawa Bihoga
19 Aprili 2024

Israel imeapa kujibu mashambulizi ya Iran ya mwishoni mwa juma ambayo yamesababisha hofu ya kutanuka kwa mzozo, baada ya miezi kadhaa ya mapigano yaliosababisha maelfu ya watu kuuwawa Gaza.

Israel, Tel Aviv | Baraza la vita likiwa katika kikao chake
Baraza la vita la Israel likiwa katika kikao baada ya shambulio la IranPicha: Israeli Government Press Office/Anadolu/picture alliance

Washirika wa Israel wamekuwa wakiitaka kujizuia kufuatia shambulio hilo la Iran ambayo kwa sasa viongozi wa Umoja wa Ulaya wameapa kuongeza mbinyo wa vikwazo dhidi yake wakilenga usafirishaji wake wa ndege zisizo na rubani na makombora kwa washirika wake wa Ukanda wa Gaza, Yemen na Lebanon.

Marekani ambayo nayo iliweka vikwazo ambavyo vimelenga watu binafsi pamoja na wazalishaji wa zana hizo. mashambulizi ya Iran siku ya Jumamosi, yaliashiria mara ya kwanza kwa Tehran kufanya shambulio la kijeshi na la moja kwa moja dhidi ya Israel.

Soma pia:Kwanini Iran na Israel ni maadui?

Mamlaka ya Israel ilisema Iran ilirusha zaidi ya makombora na droni 300 na asilimia 99 ya mashambulizi hayo yalizuiliwa na mifumo ya ulinzi wa anga wakishirikiana na Marekani, Uingereza, Ufaransa na Jordan.
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW