1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIsrael

UN yapitisha azimio la kufikishwa misaada ya kiutu Gaza

28 Oktoba 2023

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa limeidhinisha azimio lisilo na uzito wa kisheria linalotaka "makubaliano ya mara moja, ya kudumu na endelevu ya kibinadamu" katika Ukanda wa Gaza.

Mashambulizi ya makombora ya Israel yameligubika eneo la Gaza na kuibua kitisho kikubwa cha janga la kiutu kwenye eneo hilo
Mashambulizi ya makombora ya Israel yameligubika eneo la Gaza na kuibua kitisho kikubwa cha janga la kiutu kwenye eneo hiloPicha: AFP

Mataifa 120 yameunga mkono azimio hilo lililoandaliwa na Jordan na kuungwa mkono na mataifa 22 ya Kiarabu. Mataifa 14 yalipinga azimio hilo ikiwa ni pamoja na Israel, Marekani na Australia. Mataifa 45 hayakupiga kura na Ujerumani, Italia na Uingereza yalijizuia.

Azimio hilo limetaka kufikiwa kwa makubaliano ya haraka ili kuruhusu misaada kuingia Gaza pamoja na kusitishwa kwa mapigano.

Israel imekosoa kwa ghadhabu pendekezo hilo, huku balozi wake kwenye Umoja wa Mataifa Gilad Erdan akiliita "takataka" na kusema Israel itaendelea kujilinda huku Hamas na Palestina wakilikaribisha.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW