1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIsrael

Israel imepitisha sheria itakayomlinda Netanyahu

23 Machi 2023

Bunge la Israel limepitisha sheria ya mwanzo kati ya kadhaa zinazokusudia marekebisho ya mahakama yenye utata.

Israel Tel Aviv | Protest von Reservisten
Picha: Oded Balilty/AP/picture alliance

Sheria hiyo imepitishwa huku waandamanaji wanaopinga mageuzi hayo wakiendeleza maandamano ya kupinga kile wanachokiona kuwa ni mwelekeo wa taifa kwenye utawala wa kimabavu.

Muungano wa Waziri mkuu Benjamin Netanyahu umeridhia sheria itakayomlinda kiongozi huyo wa  Israel asionekane kuwa hafai kutawala kutokana na kesi yake ya rushwa na madai ya mgongano wa kimaslahi kuhusiana na ushiriki wake katika mabadiliko ya sheria.

Mabadiliko ya kisheria yamegawanya taifa kati ya wale wanaoiona sera mpya kama kuiondolea Israeli maadili yake ya kidemokrasia na wale ambao

wanadhani nchi imetawaliwa na uhura wa kimahakama.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW