1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIsrael

Urusi na China zapinga azimio la UN juu ya Israel

26 Oktoba 2023

Urusi na China zimepigia kura ya turufu muswada wa azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusiana na vita vya Israel dhidi ya kundi la Hamas katika Ukanda wa Gaza.

Pichani ni wanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa katika kikao cha kupigia kura muswada wa azimio la usitishwaji wa vita vya Israel dhidi ya Hamas
Pichani ni wanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa katika kikao cha kupigia kura muswada wa azimio la usitishwaji wa vita vya Israel dhidi ya Hamas Picha: David Dee Delgado/REUTERS

Muswada huo ulioandaliwa na Marekani ulizungumzia namna ya kushughulikia mzozo wa kibinaadamu unaozidi kuwa mbaya katika eneo la Gaza na kutoa wito wa kusimamishwa mapigano ili kuruhusu upitishwaji wa misaada.

Umoja wa Falme za Kiarabu pia uliupinga muswada huo, huku wanachama 10 wakiukubali. Brazil na Msumbiji hawakuupigia kura.

Urusi pia iliandaa muswada wa azimio la usitishwaji wa mapigano wa kiutu, lakini haukupata uungaji mkono unaotakiwa. Ni mataifa manne tu yaliyoupigia kura huku Marekani na Uingereza yakiupinga.