Israel: Bado hakuna makubaliano ya kuachiliwa mateka
19 Novemba 2023Mateka hao wanashikiliwa na wanamgambo wa Hamas na makubaliano yangewezesha kuachiliwa kwa idadi kubwa ya mateka wanawake na watoto.
Hii ni baada ya gazeti la Washington Post la Marekani kuripoti kwamba Israel na Hamas wamekubaliana kusitisha mapigano kwa muda wa siku hizo tano ili kuruhusu mchakato huo.
Netanyahu amewaambia waandishi wa habari katika mkutano jana jioni ambapo alisisitiza kwamba hakuna makubaliano yaliyofikiwa hadi sasa na ameahidi kutoa taarifa patakapokuwa na jambo lolote.
Msemaji wa masuala ya usalama wa taifa wa Ikulu ya Marekani, Adrienne Watson pia amezipuuza ripoti hizo na kuandika kupitia ukurasa wake wa X kwamba makubaliano hayo hayajafikiwa, ingawa wanaendelea na jitihada.
Hamas, waliposhambulia kusini mwa Israel, mnamo Oktoba 7 walichukua mateka watu 240 na watu wengine 1,200 waliuawa.