Israel inakumbuka wanajeshi waliokufa na wahanga
25 Aprili 2023Matangazo
Siku ya Ukumbusho ni moja ya nyakati muhimu zaidi katika kalenda ya kitaifa ya Israel, inayotoa heshima kwa askari 24,213 waliouawa vitani na wahanga 4,255 wa mashambulizi.Israel wakati huu inapitia migawanyiko mkubwa kuhusiana na mpango tata wa serikali ya Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu, wa kuifanyia mabadiliko mapana idara ya mahakama. Mwaka huu, Israel inaadhimisha miaka 75 ya kuanzishwa kwake. Aidha, hayo yanafanyika wakati ambapo Israel na Wapalestina katika Ukingo wa Magharibi wanakabiliana katika mojawapo ya machafuko makali zaidi kuwahi kushuhudiwa katika eneo hilo kwa miaka mingi.