1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel inapanga kuanzisha operesheni ya ardhini Lebanon

26 Septemba 2024

Israel imesema kuna uwezekano wa kuanzisha operesheni ya ardhini huko Lebanon.

Mkuu wa majeshi ya ulinzi wa Israel Herzi Halevi
Mkuu wa majeshi ya ulinzi wa Israel Herzi HaleviPicha: Israeli Defense Forces/IDF/dpa/picture alliance

Mkuu wa majeshi ya ulinzi wa Israel Herzi Halevi, amesema mashambulizi makali yanayoendelea nchini Lebanon ni kwa ajili ya kuandaa uwezekano wa operesheni ya ardhini dhidi ya kundi la  Hezbollah . Kauli hii inajiri siku moja baada ya kundi hilo kuvurumisha makombora ndani ya Israel.

Hayo yanajiri wakati jumuiya ya kimataifa ikijaribu kuzuia kutanuka kwa mzozo huo, Marekani na Ufaransa wamependekeza usitishwaji mapigano kwa muda wa siku 21 ili kuwaruhusu kuandaa makubaliano ya kusitisha vita na kusimamia mpango wa mazungumzo mapana zaidi ambayo yataijumuisha pia Gaza.

Hata hivyo Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu aliapa kwamba operesheni za kijeshi za Israel dhidi ya Hezbollah hazitasitishwa hadi wakaazi wa kaskazini waliokimbia makazi yao kutokana na mapigano hayo waweze kurejea salama makwao.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW