1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIsrael

Israel kuchukua hatua baada ya Palestina kwenda ICJ

6 Januari 2023

Israel imesema kuwa itazuia ujenzi wa baadhi ya makaazi ya Wapalestina na kutumia fedha za Palestina kuwalipa fidia wahanga wa ugaidi wa Israel.

BdT Palästina Küstenerosion in Gaza bedroht Strandcafés und Straßen
Picha: Mohammed Salem/REUTERS

Uamuzi huo ni katika kujibu hatua ya Palestina kukata rufaa katika Mahakama ya Haki ya Kimataifa, ICJ.

Ofisi ya Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu imesema leo kuwa hatua hizo ni kujibu uamuzi wa Mamlaka ya Palestina ya kuanzisha vita vya kisiasa na kisheria dhidi ya taifa la Israel.

Kutokana na rufaa ya Wapalestina, wiki iliyopita Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa liliiomba mahakama ya ICJ kutoa maoni yake kuhusu madhara ya kisheria kutokana na Israel kuikalia kimabavu ardhi ya Wapalestina kwa miaka 55.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW