1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel kupunguza askari wake kutoka kwenye Ukanda wa Gaza

2 Januari 2024

Jeshi la Israel limethibitisha kuwa litawaondoa wanajeshi wake kutoka kwenye Ukanda wa Gaza, hatua ambayo inaweza kufungua njia ya awamu mpya ya mapigano ya viwango vya chini lakini ya muda mrefu dhidi ya Hamas.

Askari wa Israel katika Ukingo wa Magharibi
Askari wa Israel katika Ukingo wa MagharibiPicha: Ammar Awad/REUTERS

Jeshi la Israel limethibitisha kuwa litawaondoa maelfu ya wanajeshi wake kutoka kwenye Ukanda wa Gaza, hatua ambayo inaweza kufungua njia ya awamu mpya ya mapigano ya viwango vya chini lakini ya muda mrefu dhidi ya wapiganaji wa kundi la Hamas. Jeshi la Israel ladai kuharibu maficho ya wanamgambo wa Hamas huko Gaza

Kuthibitishwa mpango huo wa kupunguza askari, kumefahamika siku ambapo mahakama ya juu ya Israel ilitupilia mbali kipengele muhimu, cha mageuzi ya sheria yanayotetewa na waziri mkuu Benjamin Netanyahu.

Ingawa mpango huo hauhusiani na vita vinavyoendelea lakini umekuwa chanzo cha migawiko mikubwa nchini Israel na ulitishia utayarifu wa majeshi ya nchi hiyo kabla ya tarehe 7 Oktoba ambapo wanamgambo wa waliishambulia Israel. Marekani, Umoja wa Ulaya na nchi nyingine kadhaa zimeliorodhesha kundi la Hamas kama kundi la kigaidi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW