Israel kurekibisha ukuta wake mpakani
21 Februari 2004Matangazo
JERUSALEM: Israel inataka kubomoa kilomita 9 za ukuta wake mkabala wa Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan. Kazi za kubomoa zitaanza Jumapili ya kesho, iliarifu Wizara ya Mambo ya Ulinzi ya Israel. Marekibisho hayo yamekusudiwa kuwarejeshea Wapalestina kijiji cha Baka as Sharkia kilichomezwa na ujenzi wa ukuta huo. Hapo Jumatatu, mjini The Hague, yataanza kusikilizwa mashtaka rasmi yaliyopelekwa na Baraza Kuu la UM kuhusu haki ya kujengwa ukuta huo. Hapo jana Shirika la Kimataifa la Haki za Binadamu Amnesty International hapo lililaumu kuwa ujenzi wa ukuta wa Israel unakiuka Sheria za Kimataifa. Urefu wa KM 200 zilizokwisha jengwa zinaingia ndani mno ya ardhi za Wapalestina. - Wanajeshi wa Israel wamempiga risasi na kumwua Mpalestina karibu ya makazi ya Kiyahudi kwenye Mkanda wa Ghaza.
