1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel kushambulia kambi ya Nuseirat kaskazini mwa Gaza

Sylvia Mwehozi
12 Januari 2025

Jeshi la Israel limesema hii leo kuwa litashambulia kambi ya wakimbizi ya Nuseirat iliyopo kaskazini mwa Ukanda wa Gaza.

Wapalestina katikati mwa vifusi huko Gaza
Wapalestina katikati mwa vifusi huko GazaPicha: Moiz Salhi/Anadolu/picture alliance

Jeshi la Israel limesema kuwa litashambulia kambi ya wakimbizi ya Nuseirat iliyopo kaskazini mwa Ukanda wa Gaza, na kuwataka raia kuondoka haraka eneo hilo na kuelekea katika eneo la kibinaadamu kwa usalama wao.

Msemaji wa lugha ya kiarabu wa Jeshi la Ulinzi la Israel (IDF) Avichay Adraee ameandika kwenye ukurasa wa mtandao wa kijamii wa X kwamba roketi zilifyatuliwa kuelekea Israel, kutoka kambini hapo na kwamba shambulio la Israel linakaribia.

Vita vya Gaza vilianza Oktoba 7 mwaka 2023 baada ya wanamgambo wa Hamas kuvamia kusini mwa Israel na kuua watu 1,200 na kuwachukua mateka wengine zaidi ya 200.Hamas yathibitisha kuanza kwa mazungumzo ya kusitisha vita Gaza

Mashambulizi ya kulipiza kisasi ya Israel tayari yamesababisha vifo vya watu zaidi ya 46,000 huko Gaza kulingana na wizara ya afya ya Hamas inayodhibiti eneo hilo.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW