1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel kutanua malengo yake ya vita kuijumuisha Lebanon

Josephat Charo
17 Septemba 2024

Israel imetangaza leo nia ya kuvitanua vita vyake, kupanua vita vilivyodumu karibu mwaka mmoja dhidi ya Hamas katika Ukanda wa Gaza na kuelekeza nguvu dhidi ya Hezobollah katika mpaka wake wa kaskazini na Lebanon.

Ukanda wa Gaza | Athari za mashambulizi ya Israel.
Majengo yaliobomolewa Gaza baada ya mashambulizi ya Israel.Picha: Omar Ashtawy/APAimages/IMAGO

Tangazo hilo limetolewa huku waziri wa mambo ya nje wa Marekani Anthony Blinken akitarajiwa kuzuru eneo hilo wiki hii kuyafufua mazungumzo yaliyokwama yanayonuiwa kusitisha vita kati ya Israel na Hamas huko Gaza.

Soma pia:Israeli yaongeza masharti katika vita vya Gaza

Kufikia sasa nia ya Israel imekuwa kulisambaratisha kabisa kundi la Hamas na kuwarejesha nyumbani mateka waliochukuliwa na wanamgambo wa Kipalestina wakati wa shambulizi la Oktoba 7 mwaka uliopita lililozua vita hivyo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW