1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiIsrael

Israel kuwaruhusu wafanyakazi wa Gaza kupita

28 Septemba 2023

Israel imeufunguwa tena mpaka wake na Ukanda wa Gaza kuwaruhusu maelfu ya wafanyakazi wa Kipalestina kuingia kwenye nchi hiyo pamoja na Ukingo wa Magharibi, wiki moja baada ya kuufunga.

Israel kuwaruhusu wafanyakazi wa Gaza kupita
Israel kuwaruhusu wafanyakazi wa Gaza kupitaPicha: Tania Krämer/Dw

Israel imeufunguwa tena mpaka wake na Ukanda wa Gaza kuwaruhusu maelfu ya wafanyakazi wa Kipalestina kuingia kwenye nchi hiyo pamoja na Ukingo wa Magharibi, wiki moja baada ya kuufunga.

Mpaka huo umefuguliwa tena baada ya wiki kadhaa za machafuko, ambapo waandamanaji wenye hasira wa upande wa Gaza, walikabiliana na vyombo vya usalama.

Kufunguliwa kwa kivuko hicho kunatokana na juhudi za kimataifa zikiongozwa na Misri na Umoja wa Mataifa.

Haijulikani kivuuko cha Erez kitasalia wazi kwa muda gani, kwani mapumziko ya wiki moja ya jamii ya Kiyahudi yanaanza kesho Ijumaa, na kawaida, Israel huwa inafunga vivuko vyote wakati wa mapumziko.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW