1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel- Hamas warefusha makubaliana ya kusitisha mapigano

28 Novemba 2023

Israel na kundi la wanamgambo la Hamas wamekubaliana kuongeza muda wa kusitisha mapigano hadi kesho Jumatano, na kuongeza matarajio ya mabadilishano zaidi ya mateka na wafungwa.

Askari wa Israel akielekea katika oparesheni
Askari wa Israel akielekea katika oparesheniPicha: Kahana/AFP

Wanawake 11 wa Israel pamoja na watoto waliochiliwa huru na Hamas waliingia Israel jana usiku baada ya zaidi ya wiki saba mikononi mwa Hamas.

Kwa upande mwengine, wafungwa 33 wa Kipalestina walioachiliwa na Israel wamewasili mapema leo mashariki mwa Jerusalem na mji wa Ramallah ulioko ukingo wa Magharibi. Wafungwa hao wamekaribishwa kwa shangwe wakati basi lililowabeba lilipokuwa linapita barabarani mjini Ramallah.

Soma pia:Usitishaji vita waibua matumaini ya mateka zaidi kuachiwa

Makubaliano hayo ya siku mbili za ziada za kusitisha mapigano yameibua matumaini ya kuongeza muda zaidi wa usitishwaji mapigano, hali ambayo itaruhusu misaada zaidi katika ukanda wa Gaza ambao umekabiliwa na wiki za mashambulizi ya Israel.


Mashambulizi hayo yamesababisha zaidi ya watu milioni 2.3 kuyahama makaazi yao.