1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel na Hamas wapambana karibu na hospitali mbili Gaza

9 Novemba 2023

Israel imeushambulia mji wa Gaza kwa makombora leo huku vikosi vyake vya ardhini vikipambana na wanamgambo wa Hamas karibu na hospitali mbili ambazo zinawahifadhi maelfu ya Wapalestina wanaokimbia mapigano.

Jeshi la Israel likiendeleza oparesheni yake katika ukanda wa Gaza
Jeshi la Israel likiendeleza oparesheni yake katika ukanda wa GazaPicha: Israel Defense Forces/Handout via REUTERS

Duru zinasema vikosi vya Israel vikisaidiwa na ndege za kivita vinakabiliana na wapiganaji wa Hamas jirani na hospitali za Al Shifa na Al-Quds zilizopo kaskazini mwa Ukanda wa Gaza eneo ambalo ndiyo kitovu cha operesheni ya Israel.

Jeshi la nchi hiyo limesema kamandi kuu ya kundi la Hamas imo ndani na chini ya hospital ya Al-Shifa madai ambayo yamekanushwa na kundi hilo pamoja na wafanyakazi wa hospitali hiyo.

Makabiliano kwenye mji huo mkubwa wa Ukanda wa Gaza yanaendelea wakati miito inaongezeka ya kutafutwa mwafaka wa usitishaji vita kwa muda  ili kuwasaidia mamilioni ya Wapalestina wanaokabiliwa na ukosefu wa mahitaji muhimu.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW