1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel na Iran zaanzisha mashambulizi mapya ya kila upande

2 Machi 2026

Israel na Iran zimeanzisha mashambulizi mapya dhidi ya kila upande leo Jumatatu, huku Tehran ikiripotiwa kurusha makombora kuelekea Israel, na Jeshi la Anga la Israel likishambulia maeneo mjini Tehran.

Eneo la Beit nchini Israel lililoharibiwa na shambulio la makombora ya Iran-Machi 2, 2026
Iran imerusha makombora mengi dhidi ya Israel baada ya Marekani na Israeli kuanzisha shambulio la pamoja dhidi ya IranPicha: Alexi J. Rosenfeld/Getty Images

Israel na Iran zimeanzisha mashambulizi mapya dhidi ya kila upande leo Jumatatu, huku Tehran ikiripotiwa kurusha makombora kuelekea Israel, na Jeshi la Anga la Israel likishambulia maeneo mjini Tehran.

Jeshi la Israel limesema Iran ilirusha tena makombora asubuhi, na mifumo ya ulinzi wa anga ilikuwa ikifanya kazi kuyazuia. Ving'ora vya tahadhari vilisikika mjini Tel Aviv na maeneo mengine, huku wakazi wakitakiwa kujihifadhi katika maeneo salama.

Iran imekuwa ikilenga adui wake mkuu kwa makombora tangu kuuawa kwa kiongozi wake mkuu Ali Khamenei katika mashambulizi ya anga ya Israel na Marekani Jumamosi.

Kwa mujibu wa Israel, operesheni ya jeshi lake la anga dhidi ya Iran, iliyoanzishwa Jumamosi asubuhi kwa uratibu na mshirika wake Marekani, ndiyo kubwa zaidi katika historia yake hadi sasa.

Jeshi la Marekani pia limesema lina nia ya kuendelea na operesheni zake nchini Iran.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW