1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel na Lebanon zakubaliana kuandaa mazungumzo mengine

15 Aprili 2026

Israel na Lebanon zimekubaliana kufanya mazungumzo mapana ya ngazi ya juu baada ya pande hizo mbili kukutana kwa mara ya kwanza kwa mashauriano ya awali mjini Washington jana Jumanne.

Lebanon Beirut 2026 | Waziri Mkuu wa Lebanon Nawaf Salam
Waziri Mkuu wa Lebanon Nawaf Salam.Picha: Mohamed Azakir/REUTERS

Tangazo hilo limetolewa baada ya kukamilika kwa mashauriano hayo yaliyodumu kwa zaidi ya saa mbili kati ya wawakilishi wa Israel na Lebanon chini ya upatanishi wa Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Marekani, Marco Rubio.

Ofisi ya Rubio imesema pande zote mbili zimekubaliana kufanya mazunungumzo ya moja kwa moja katika eneo na muda utakaoafikiwa kwa pamoja.

Hayo yalikuwa mashauriano ya kwanza kati ya nchi hizo mbili jirani ambazo zimetumbukia kwenye uhasama wa muda mrefu kutokana na harakati za kundi laHezbollah la nchini Lebanon lenye mafungamano ya karibu na Iran. Israel imesema inataka kushirikiana na serikali ya Lebanon kulipokonya silaha kundi hilo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW